Tuesday, May 20, 2014

NEW HIT SONG Mawazo by Davos'

Mwazo ni wimbo mpya ulioimbwa  na  Msanii wa kizazi kipya anayekwenda kwa jina la DAVOS' akifanya maojiano na mwaandishi wa bongojotolinkblog alisema kuwa amejipanga vema kukabiliana nachangamoto zinazojitokeza kwenye muziki wetu wa bongofleva pia alimalizia kusema  anaamini bila ya kufight hakuna mafanikio mwisho akamalizia kwa kuomba support  yako ukiwa kama mdau au mpenzi wa muziki wa kizazi kipya kutoka hapa nyumbani Tanzania.. Na endapo utamsikiliza vizuri kwenye huu wimbo utagundua kuna kitu cha ziada ndani yake kuanzia uwandishi na umahiri katika kupangilia sauti...


DAVOS'

  

Monday, May 19, 2014

Wimbo NADATA NA WEWE umekuwagumzo mtaani..


Ile ngoma iliyokuwa inasubiriwa kwa hamu kupitia msanii nguli wa bongo fleva ambae anafanya vizuri kwa sasa namzungumzia Ally Kasongo Ram jina la kisanii  RAMLIFE imekuwa gumzo mtaani kutokana na kupokelewa vizuri na wadau wa burudani kupitia vyombo mbalimbali vya habari ngoma hiyo aliyoirekodi katika studio za Gofu Rec. zilizopo maeneo ya mwananyamala kwa makoma chini ya mtayarishaji mahiri Kaju inajulikana kwa jina la "Nadataawe"
ambapo mashabiki wengi wamempokea kwa taharuki msanii huyu sababu ya uwezo wake mkubwa wa kuimba na kutunga mashairi yenye hisia ambayo yanapendwa na wadau wengi kwa sasa
Akizungumza na BongojotoLink jemedali huyo alitanabaisha kwamba hizi ni cheche tu za safari yake yenye moto mkubwa anawashukuru sana wote waliomsapoti na wanaomsapoti anachowahaidi ni zawadi ya burudani isiyosadikika.


  RAMLIFE
RAMLIIFE



 
Hii ni moja ya Snap shot ya video "NADATA NA WEWE"

Sunday, September 22, 2013

PICHA ZAIDI ZA TUKIO LA MAJAMBAZI KUVAMIA SUPERMARKET KENYA

TUKIO hili la uvamizi limetokea huko Westlands Nairobi nchini Kenya, Ni sehemu inayoishi wakenya wenye asili ya kihindi, mall inaitwa westagate.
 


Thursday, May 9, 2013

KUMPIGIA KURA STAMINA Kili Music Awards

                                                         
                                                        VOTE LINK

Tuesday, October 16, 2012

E MEDIA NA IZZO B TENA...!




Nguli wa muziki wa kufokafoka kutoka jijini mbeya anaetamba na mkwaju wa Riz one muite Izzo B njiani kuachia ngoma yake mpya ikiambatana na video, sindano hiyo imetaarishwa na kampuni ya E MEDIA chini ya mkali Nick Dizzo, usikae mbali na tovuti yako kwa video kali..

WASANII 3 WANAOMNYIMA USINGIZI MKALI DITO..

 Yule mkali kutoka nyumba ya vipaji Tanzania House Of  Talent a.k.a THT. anaesifika kwa sauti yenye hisia na mashairi ya kufundisha wanamuita Dito, amefunguka kupitia tovuti hii kuwa wasanii wa 3 wa Bongo anaowazimia ni mkongwe  Pro J, Gwiji wa muziki wa Afrika mashariki hayati Marijani Rajabu pamoja na aliekuwa msanii mwenzake katika kundi moja mkali kutoka Mji kasoro bahari {Morogoro}Afande sele, Msanii Dito ametamba na ngoma kali kama vile Wapo, Tushukuru kwa yote pamoja na Niamini.

Tuesday, June 19, 2012

MBUNGE WA JIMBO LA UBONGO, JOHN MNYIKA ATOLEWA BUNGENI LEO

Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka nje ya viwanja vya  Bunge la Tanzania leo mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.

Mbunge wa Jimbo la Ubungo John Mnyika akiteta na Mbunge wa jimbo la Wawi Hamad RashidMohamed (kushoto) na Mbunge wa Bariadi Mashariki John Cheyo  mara baada ya kuondolewa Bungeni jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendelea.

Mbunge wa jimbo la Ubungo John Mnyika akitoka katika ukumbi wa Bunge la Tanzania jana mjini Dodoma baada ya kukataa kufuta kauli ya kumdhalilisha Rais wa Jamhuri ya  Muungano wa Tanzania kuwa dhaifu. Mbunge huyo alitoa kauli hiyo wakati akichangia Bajeti ya serikali ya mwaka 2012/13 katika mkutano unaoendele

Sunday, June 10, 2012

MKUTANO WA CCM JANGWANI JANA

Waziri wa Ujenzi, John Magufuli, akienda kuhutubia.


Waziri wa Uchukuzi, Harrison Mwakyembe, akiwahutubia wananchi.
 
Waziri wa Nyumba na Makazi, Prof. Anna Tibaijuka akienda kuhutubia.…



 


Monday, May 28, 2012

SAJUKI, MWACHENI MUNGU AITWE MUNGU !!!!

Sajuki akiwa amepumzika, pembeni ni mkewe Wastara Juma.

                      















                          Sounce: globalpublisher
                              Sounce link : globalpublisher





Tuesday, May 22, 2012

FAHAMU ALIPOKULIA MAREHEMU KANUMBA NA MWIGIZAJI JOHARI

NYUMBANI ANAPOISHI BABA YAKE KANUMBA PAMOJA NA WAPANGAJI
  ..KANISA ALIPOKUWA AKISALII MAREHEMU KANUMBA NA SEHEMU ALIPOANZIA KUIGIZA AKIWA NA UMRI MDOGO SANA. INAAMINIKA KUWA PIA KANISA HILI NDIPO ALIPOKUANZA KUIGIZA  MWIGIZAJI JOHARI..

   SHULE ALIYOSOMA MAREHEMU KANUMBA PAMOJA NA MWIGIZAJI JOHARI.

Monday, May 7, 2012

Hilda and Julio washiriki wa BBA 2012 kutoka TANZANIA








Hilda

Hilda

Age 28
Country
Tanzania
Occupation Saleswoman
Biography Hilda hails from Morogoro and is a saleswoman. She has a son and enjoys the novels of Sydney Sheldon and the book Memoirs of a Geisha. Hilda was inspired to enter Big Brother StarGame by Biggie himself! “He seems to be a big challenge in the House and so I thought it would be fun to join him this time around and give him a special challenge. I can’t wait…” she says. She’s excited by the partnering format of this year’s show as it will be filled with fun and entertainment – plus her partner Julio is her best friend. “He is charming, sweet and a very good listener, of course,” she says.

She says she will do whatever it takes to win the grand prize – including lying her way out of a tricky situation or “being the sweetest thing ever”. She knows that Africa will be talking about her as soon as they see her on screen – which makes her excited. She says if she wins, she will donate money to a charity she supports back home as a peer health educator to help them build a nice house.

 

 

    Julio

                           Julio

Age 27
Country
Tanzania
Occupation Manager
Biography Julio is from Dar es Salaam and works as the Head of VAS, Electronic Channels and Products at a company in the telecommunications industry. With a BComm in Finance and an MBA under his belt, he looks set to be a wily player on Big Brother StarGame! He entered to be on the show because his best friend – Hilda – was the perfect example of the best candidate. Coupled with that, he saw himself as the most complete character because of how he lives his life as a hedonist.

He says of his partner Hilda that she is “real and straightforward” and that he’s always comfortable when she’s around. He says that men adore her while women are always on his case. “She’s smart, very interesting – especially with how much she knows, Africa will love her to death,” he says. He’s a fan of the show and cites Kevin as his favourite Housemate, though he says “at the end of the day, he has nothing on what I’ll bring to the House”.


Julio describes himself as fun, crazy, smart, cunning and entertaining.

Sunday, May 6, 2012

Mwandishi wa Kitabu cha STEVEN KANUMBA - Mwisho wa Enzi, Joseph Shaluwa

 
Mwandishi wa Kitabu cha STEVEN KANUMBA - Mwisho wa Enzi, Joseph Shaluwa(mwenye tai) akipokea mkataba wa kisheria kati yake na mama wa marehemu Kanumba, Flora Mtegoa, nyumbani kwa marehemu leo saa 7 mchana, Sinza, Vatican, jijini Dar es Salaam. Shaluwa amepewa mkataba huo baada ya kulipa asilimia 35 ya faida ya kitabu hicho. Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Filamu Tanzania 'TAFF' Wilson Makubi, Seth Bosco, mdogo wa marehemu na Simon Mwakifwamba, Rais wa TAFF.

Sunday, March 11, 2012

WEMA SEPETU AJIBU BAADA YA KUFANYIWA FUJO NA MKE WA MTU!

                          Hii ni moja kati ya picha alizopiga wakati alipokua akifanya shopping 
                        huko Dubai,   shopping ambayo inadaiwa alipelekwa na huyo pedeshee!
 

Baada ya kuletewa fujo weekend iliyopita na mwanamke anaedai muigizaji Wema Sepetu amemuibia mume, leo mrembo huyo (Wema) ameamua kuzungumzia upande wake ambapo kama haukuingia millardayo.com juzi march 5 kulikua na stori ya huyo mwanamke kumfanyia fujo Wema baada ya kumkuta yeye na wasanii wenzake ndani ya Pub ambayo inamilikiwa na mwanamke huyo. Wema amesema “kwanza mimi mwenyewe nilishtuka sana, nilikua natafuta location ya kucheza movie yangu kwenye mgahawa, nikawa nimepaki nje kutoka na kurudi nikamkuta mwanamke ndani ya gari jeupe limepaki pembeni yangu siijui wala huyo mwanamke simjui nikamchukulia kama mmoja wa haters, akaanza kufanya fujo wakati mimi huwa siwezi fujo, nikajitahidi kutoka eneo la tukio na kupiga simu polisi na kuja kumchukua huyo mwanamke na kwenda polisi Osterbay” “Kiukweli sitembei na mwanaume wake, sitembei na mume wa mtu……. alafu yule ni mwanamke mtu mzima sana hawezi kugombana na mimi, mi mtoto mdogo akitaka aje na uthibitisho, alafu anasema gari ninayotembela ni yake? gari ni yangu mpaka kazi ninazo mimi huo ni ujinga na ndio maana siwezi nikaachia hii kitu iende hivyo hivyo tu kama anavyotaka yeye” – Wema “Kama kweli ningekua namchukulia mwanamke wake sidhani kama ningekua nimefikishana nae hapa tulipofika manake ningekua namuogopa, sasa simuogopi na afanye chochote anachotaka kufanya, waniache na maisha yangu nimekaa kimya mtoto wa watu wananifatafata, nikisema watasema nimesema, waniache basi mi mwenyewe nina maisha yangu ya kuishi” hayo ni maneno ya Wema ambae pia amekataa na kuapa kwamba hajawahi kutumia bili za milioni 1.5 mpaka mbili kwenye baa ya huyo mwanamke, huku ikidaiwa kwamba bili hizo zimekua zikilipwa na huyo pedeshee ambae ni mume wa mwanamke mwenye pub. Jana mmoja kati ya marafiki wa Wema akiwa ni mdogo wake na mke wa pedeshee huyo, alikiri kwamba urafiki wake na Wema umevunjika baada ya kugundua anatoka kimapenzi na mume wa dada yake (yani mume wa mwanamke aliemfanyia Wema fujo)
http://millardayo.com/

Saturday, March 10, 2012

Mahakama Kuu yasitisha mgomo wa madaktari

MAHAKAMA Kuu Divisheni ya Kazi imewaagiza madaktari walioitisha mgomo nchi nzima, kuusitisha mara moja.

Mbali na kusitisha mgomo huo, madaktari hao wameagizwa kutumia vyombo vya habari ilivyotumia kutangaza mgomo huo, kuutangazia umma kwamba mgomo huo haupo tena na kwamba wanarejea kazini.

Uamuzi huo umekuja siku moja baada ya madaktari hao kuanza rasmi mgomo wao wakishinikiza kujiuzulu kwa Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya, kama moja ya sharti la kuendelea na mazungumzo na Serikali juu ya
madai yao mbalimbali ya maslahi.

Uamuzi wa Mahakama hiyo ulitolewa jana usiku na Jaji Regina Rweyemamu baada ya kusikiliza maombi ya Serikali yaliyowasilishwa mahakamani hapo Jumatano na Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema, kupinga mgomo huo uliotangazwa juzi na madaktari hao, kinyume cha utaratibu.

Katika maombi yaliyowasilishwa mahakamani juzi chini ya hati ya dharura, Jaji Werema, alidai kuwa mgomo huo ni hatari kwa maisha ya watu na unafanyika wakati majadiliano yameanza kati ya madaktari na Serikali na huku kukiwa na kesi Tume ya Usuluhishi na Uamuzi (CMA) ambayo haijamalizika.

Pia alidai kuwa mgomo ni batili kwa kuwa haukufuata utaratibu kwani madaktari hao wana kiapo cha taaluma yao, ambacho kinaeleza kuwa wao ni sehemu ya taaluma ambazo haziruhusiwi kugoma.

Awali, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alifungua kesi katika Tume ya Usuluhishi na Uamuzi, Jumanne iliyopita, lakini licha ya kupelekewa hati ya kuitwa katka shauri hilo, madaktari hao hawakutokea na zaidi ya hapo wakatangaza mgomo.

Kutokana na hilo, Serikali ililazimizika kwenda Mahakama Kuu Divisheni ya Kazi chini ya hati ya dharura juzi kuiomba izuie mgomo huo.

Mbali na kugoma, Mwanasheria Mkuu wa Serikali alidai madaktari hao walikuwa na njia za kufanya kabla ya kugoma ikiwemo, kwenda Tume ya Usuluhishi na Uamuzi au kwenda katika Kamati inayoshughulika Huduma Maalumu.

Washitakiwa katika kesi hiyo ni Chama cha Madaktari (MAT) na Jumuiya ya Madaktari ambayo
Serikali inadai kuwa ni batili kwa kuwa haijasajiliwa.

Katika kesi hiyo, Serikali iliwakilishwa na Wakili Mwandamizi, Edson Mweyunge na walalamikiwa, MAT walihudhuria katika shauri hilo.

Mwishoni mwa wiki, madaktari walitangaza kuanza mgomo juzi baada ya Serikali kukataa matakwa yao ya kujiuzulu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Hadji Mponda na Naibu wake, Dk. Lucy Nkya.

Katika hatua nyingine, Rais Jakaya Kikwete leo anatarajia kuzungumza na Taifa kupitia Wazee wa Mkoa wa Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadiki alisema jana kwenye maadhimisho ya Siku
ya Wanawake Duniani kimkoa kuwa Rais Kikwete atazungumza na Watanzania wote kupitia wazee hao na kuwataka wafungulie vyombo vya habari kumsikiliza.

“Naomba nitoe tangazo muhimu sana, wanawake wote na Watanzania wote kwa ujumla kesho
(leo) mfungue televisheni na redio zote, mumsikilize Rais Jakaya Kikwete atazungumza na Taifa kupitia Wazee wa Dar es Salaam, tafadhali mfanye hivyo,” alitangaza Sadiki aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo ya wanawake iliyofanyika kimkoa katika Viwanja vya Mnazi
Mmoja, Dar es Salaam.

Sadiki alitoa tangazo hilo kwa msisitizo mara baada ya kuhutubia hadhara hiyo ambayo pamoja na mambo mengine, yeye (RC) alizungumzia suala la mgomo wa madaktari na kuhamasisha wanawake kushiriki katika maoni ya Katiba mpya pindi mchakato utakapoanza.

RC Sadiki alisema Rais Kikwete atazungumza na wazee hao asubuhi, lakini hakueleza atakutana nao wapi wala maudhui ya kukutana nao, ingawa imekuwa ni kawaida ya kiongozi huyo wa nchi kukutana na wazee wa mikoa mbalimbali ikiwemo ya Dar es Salaam na Dodoma na kupitia kwao, huzungumzia masuala ya kitaifa.

Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu, Salva Rweyemamu alipoulizwa kuhusu Rais kukutana na wazee hao wa Dar es Salaam, alisema kama Mkuu wa mkoa ametangaza hivyo, basi anukuliwe alivyosema.

Kwa sasa, suala la mgomo wa madaktari ulioanza jana nchini kote ndilo linalogonga vichwa kwa sasa na limetokea licha ya rai ya Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu Mizengo Pinda, kuwasihi madaktari hao kutogoma kwa sababu matatizo yao yanashughuliwa.

Katika hatua nyingine, Baraza Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) na Chama cha Wafanyakazi wa Afya na Serikali Kuu (TUGHE), vimewanasihi madaktari wanaogoma na kuwataka wazingatie kiapo chao cha kuhudumia jamii na kurejea kazini.

Katibu Mkuu wa Bakwata, Shehe Suleiman Lolila, alisema jana kwamba pamoja na madaktati hao kuwa na hoja ya msingi kuhusu madai yao, jambo la msingi zaidi wangeweka maslahi ya Watanzania mbele.

“Tayari Serikali imeonesha dalili ya kuzungumza nao, kuhusu madai waliyoyawasilisha, wangetumia fursa hiyo na kurejea kazini, kwa kuwa wao bado wanabaki kuwa watu muhimu na kugoma kwao kunaweza kuleta maafa makubwa katika jamii,” alisema.

Aliwataka kuangalia kiapo chao, lakini pia kujifunza kuwa na subira wakati masuala yao yakishughulikiwa, kwani hata dini imeweka wazi kuwa mtu anapokuwa na subira hupata mafanikio na thawabu kubwa.

Katibu Mkuu wa Tughe, Ali Kiwenge, alisema mgogoro wa madaktari kwa sasa unaumiza zaidi
wananchi hasa kisaikolojia.

“Kwa sasa mtu hata ukipigiwa simu tu ukaambiwa mtoto, baba au mama anaumwa, unaanza kuwaza utafanyaje, kwa mgogoro huu nchi iko kwenye wasiwasi mkubwa bila sababu za msingi,” alisema.

Naye Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Nicholaus
Mgaya, alipotakiwa kutoa maoni na ushauri wake, alisema atazungumza na vyombo vya
habari leo kuhusu mgomo huo.

Kwa upande wa hali katika hospitali nchini, Taasisi ya Tiba ya Mifupa ya Muhimbili (MOI) jana ilisitisha huduma za wagonjwa wa nje kutokana na kupungukiwa madaktari.

Ofisa Uhusiano wa MOI, Almas Jumaa, alisema katika taasisi hiyo wameathirika sana na mgomo kwani wamebaki madaktari 10 ambao ni wakuu wa vitengo na Idara kati ya madaktari 72 waliopo.

Katika hospitali nyingine za Dar es Salaam, wagonjwa walirudishwa nyumbani na kutakiwa kurudi hospitalini baada ya kusikia kwenye vyombo vya habari kuwa huduma zimerejea.

Katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, wagonjwa walikutwa wamekaa nje kwenye viti vyao
huku ndugu wakitafuta jinsi ya kuwahamishia katika hospitali zingine za binafsi.

Aidha, RC Sadiki aliwaondoa hofu madaktari wanaoendelea kutoa huduma katika hospitali za
mkoa huo, licha ya kushinikizwa wagome, na kusema Serikali itawapa ulinzi, kwa kuwa wamekuwa wakipokea vitisho.

Aliwaomba waendelee kuokoa maisha ya Watanzania wenzao, kulingana na kiapo walichokula
kwa kuwa tayari Serikali imekubali kushughulikia madai yao hivyo kugoma si ufumbuzi.

Mikoani katika hospitali za Bugando Mwana, KCMC Moshi, Dodoma na Morogoro kulikuwa na
mgomo baridi.

SOURCE: HABARI LEO

Patients stay away as doctors` strike bites

The number of patients going to public hospitals dropped drastically yesterday as the doctors’ strike entered its second day, paralysing services at Muhimbili National Hospital and other referral hospitals.
By yesterday evening the government was yet to announce remedial measures it is planning to take to end the strike.
A survey by The Guardian in public hospitals of Muhimbili, Temeke and Amana in Dar es Salaam revealed that only a few patients were going for treatment although they were not sure of being attended to.
At the Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI), patients who had appointments were attended to and assigned to doctors but they found the consulting rooms empty.
MOI Public Relations Officer Almasi Juma said some of the services at the hospital had deteriorated because the few working doctors could not take on the additional workload.
He admitted that services for the Out Patients Department in the clinical section have been closed until further notice and that the staff was attending to patients who are admitted.
“We usually have 70 doctors at MOI, but we have remained with only 15 …this number cannot attend to all the patients,” said Almasi.
He confirmed that doctors who were working were the heads of departments and some specialists.
At Muhimbili services were also stalled with no signs of doctors attending to patients. Patients were seen roaming in the hospital premises.
MNH Public Relations Officer Aminieli Aligaesha was not available to comment on the situation. The Guardian team found the door to his office locked and his mobile phone switched off.
Marwa Chacha a resident of Kinondoni said he decided to take his mother to Regency Hospital, after failing to get attended to at Muhimbili.
He said that he is scared of losing his mother because she has not been attended to at Muhimbili.
Filbert Tarimo coming all the way from Morogoro had an appointment yesterday with a doctor for a heart checkup but he was told to go back home until further notice.
“I am really disappointed by what is happening to the health sector in the country. The government has to intervene in this matter as a lot of patients are going to die,” he said.
At Temeke hospital, no doctors were attending the admitted patients, nor were outpatients being served. Patients were seen in the premises, hoping that they may be attended to.
“I have been here for six hours now, but there is no hope of getting any service from the doctors… I don’t know where to go. The nurses advised me to go back home if I got tired,” said Lucy Myamba who resides in Mbagala Kizuiani.
An expectant mother identified as Fatma Rashid (46) from Mtoni Kijichi who was sitting at OPD for several hours said she was waiting for admission to the maternity ward but she was told that there was no one to attend to her.
“I don’t understand what to do. I’ve been here for hours now, but they told me to go back home or find an alternative hospital,” said Fatma.
The Guardian tried to reach the Temeke Hospital Medical Officer in charge for comment, but was told they were in a meeting.
At Amana hospital in Ilala Municipality, the number of patients at the hospital had gone down drastically compared to normal days.
One of the patients who preferred anonymity said that they have been told by the OPD receptionists to wait since there was only one doctor to attend all of them and admitted patients as well.
Only two doctors were serving maternity and pediatric wards.
The Hospital Medical Officer Meshack Shimwela declined to respond to questions from journalists.
Meanwhile in Iringa region the doctors were at the hospital premises but did not attend to patients.
Surveys conducted at Iringa, Jumbo district hospitals and Makambako health centre found long queues of patients who were not sure of getting attended to at the hospitals.
“The situation here has become worse …I came here since morning, but it is now half past 2 and I have not seen a single doctor attending to patients …I call upon President Jakaya Kikwete to urgently intervene because the lives of innocent people are in danger,” said Deo Mlimwila, a resident of Ubena.
Doctors and nurses at Tanga’s Bombo hospital opted for go-slow yesterday where by they were seen roaming around the hospital wards but they didn’t provide any service to patients.
"The go-slow started today (yesterday) because I came here on Wednesday and I was attended to, but today every doctor is busy with his/her own business. They are not even looking at us,” said one of the patients who were at the reception waiting to be attended.
Some patients who went to the hospital described the doctors’ strike as a “national disaster” saying that besides causing inconvenience to patients it also threatened the lives of low income earners.
The Medical Association of Tanzania chairman Dr Namala Mkopi said on Wednesday that doctors had resolved to call a countrywide strike after the government failed to heed their call to remove Minister for Health and Social Welfare Dr Hadji Mponda and his deputy Dr Lucy Nkya.
The government on Tuesday defended Dr Mponda and Dr Nkya saying they were still new in the government and thus had nothing to do with the doctors’ problems.
“We have waited for long for the minister and his deputy to be sacked, since this issue doesn’t need a budget but decision,” said Mkopi, stressing that they will only resume work after the minister and his deputy resign or are fired.


SOURCE: THE GUARDIAN
 

Monday, February 27, 2012

Country boy NA Stamina kufanya bonge la shoo MOROGORO.


kama kawa ni wale wale vijana hatari tanzania country boy na stamina ijumaa hii ndani ya club 4 starz watapiga show kali wakisindikizwa na mabeste na richard mavoko,wajanja wote wa moro tukutane paleeeeeeeeeeee katiiiiiiiiiiiii...

Wednesday, February 22, 2012

Chris Brown na Rihanna warudiana kwa Collabo!


(Chris na Rihanna wakiwa studio)
Chris Brown na Rihanna wamewashock Fans wao baada ya kuja pamoja kwa ajili ya kushirikiana kimuziki kwa mara ya kwanza tangu uhusiano wao kuharibika vibaya. Rihanna amabaye jana alisheherekea birthday yake ya kutimiza miaka 24, aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter kwa kuiimba nyimbo yake mpya na Chris Brown, Cake remix.
Chris naye alimwish ex wake huyo Happy Birthday humo humo kwenye ukursasa wa Twitter amabamo Rihanna baadaye alimshukuru mpenzi wake huyo wa zamani.

Picha ya kwanza ya Mtoto wa Jay Z

Wadau, Familia ya The Carters, Jay Z na Mkewe Beyonce wamerelease picha za kwanza za mtoto wao Blue Ivy Carter.
Wengine wamedai mtoto amezidi uweupe lakini bado mchanga so tutamsubiri tuchek.
She is a stronger faster Bey and Jay just like baba alivyomuimba mwanao katika Glory.

Amini amefukuzwa THT, anataka kujitoa ama yote ni uzushi?!


Kuna habari kwamba mwanamuziki wa kizazi kipya Amini Mwinyimkuu ‘Amini’ amejitoa katika kundi la Nyumba ya Vipaji Tanzania THT, huko wengine wakisema kwamba msanii huyo anaweza akafukuzwa kutokana na utovu wa nidhamu…Nani yupo sahihi? Ama yote ni mbinu ya kujipandisha chati katika habari?
Baada ya kumtafuta Amini, msanii huyo alifunguka na Bonog5.com na kusema kwamba jambo hilo ataliweka wazi hivi karibuni pindi atakapofanya uzinduzi wa nyimbo yake mpya itakayokwenda kwa jina la Ni Wewe. Aliongeza kwa kusema kwamba kuhusu yeye
na THT, bado itabakikuwa kitendawili kwakuwa muda wa kuliongelea haujafika, kwani anategemea kila kitu atakiweka hadharani siku hiyo.

Kumbuka amini ni miongoni mwa wasanii wakubwa wa THT, ambaye alishawahi kuwatungia wasanii mbalimbali wa kundi hilo akiwemo Mwasiti na wengine kuwapa ushauri na hata kuwasaidia katika kutafuta sauti ya wimbo.
Pia alishawahi kuwa na uhusiano na mwanamuziki mwenzake wa kundi hilo Linah.
Swali watu bado wanajiuliza juu ya kuhama kwake THT, ni kweli? Kwa nini? Wapi anatarajia kwenda?

Ruge, Sugu wamaliza tofauti

MBUNGE wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi na Mkurugenzi wa Clouds Media, Rugemalila Mutahaba jana walitangaza kumaliza tofauti zao zilizodumu kwa zaidi ya miaka miwili baada ya kufanyika kwa vikao vya usuluhishi.

Kikao cha mwisho cha upatanishi kilifanyika jana na kuratibiwa na Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Emmanuel Nchimbi pamoja na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.


Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Waziri Nchimbi ambaye alifuatana na Ruge na Sugu, alisema katika upatanishi huo pande zote mbili ziliridhika kuwa msingi wa mgogoro wao ni kila upande kuwa na kundi la wasanii na kuamini upande mmoja hautendei haki upande mwingine.


Alisema pande hizo mbili pia ziliridhika kwamba mgogoro huo baina yao badala ya kuimarisha upatikanaji wa haki za wasanii unadhoofisha jitihada hizo.


“Pande hizo ziliridhika pia kuwa mgogoro baina yao unajenga uhasama na utengano mkubwa miongoni mwa wasanii ambao wanapaswa kuungana kudai na kusimamia maslahi yao, hivyo Mbilinyi na Mutahaba wamekubaliana mambo manne,” alisema Waziri Nchimbi.


Aliyataja makubaliano hayo kuwa ni pamoja na kumaliza mgogoro na uhasama baina yao kuanzia jana, watashirikiana kufanikisha haki na jitihada ya kuinua maslahi ya wasanii na kuwaomba watu wote wanaowaunga mkono wamalize uhasama na kufungua ukurasa mpya na ushirikiano baina yao.


Pia alisema Mbilinyi na Mutahaba wamekubaliana kufanya jitihada ya pamoja ya kuunganisha vyama vya wasanii vya Tuma na TFU ili kutetea maslahi ya wasanii wakiwa na umoja zaidi.


Kwa upande wake, Mbilinyi alikiri kuwepo kwa vita ya muda mrefu baina yao ambapo alisema anaamini vita yenye malengo mwisho wake lazima ifikie suluhu kama walivyofanya wao.


Naye Mutahaba alishukuru hatua waliyofikia na kusema kuwa inawezekana walivyokuwa wakivutana nayo yanazidi kudhoofisha tasnia ya wasanii hivyo wameamua kuachana nayo na kusonga mbele kutetea haki za wasanii.


Hata hivyo alisema atahakikisha nyimbo za wasanii zinapigwa katika vyombo vyake kwa usawa ili kuhakikisha mianya kama uonevu na rushwa havina nafasi.

Sunday, February 12, 2012

WHITNEY HOUSTON AFARIKI DUNIA

 
Msanii mkongweWhitney Elizabeth Houston amefaliki February 11, 2012,kifochake kimetokea Beverly Hilton Hotel huko Beverly Hills, California.Whitney Houston amefaliki akiwa na miaka 48,alizaliwa August 9, 1963 huko Newark, New Jersey, U.S.sababu ya kifo aijajulikana bado lakini inasadikika kuwa ni drug overdose. but uchunguzi unaendelea zaidi...   tutamkumbuka  Witney kwa wimbo wake  I will always love you! "Mungu ailaze roho yake mahali pema peponi" 

Tuesday, January 24, 2012

Street Winner Botiq

                                    street winner botiq........tupo mwenge..